Haafidhw Ibn Hajar al-´Asqalaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:
7 – Mama wa waumini Hafswah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Yule asiyelaza nia kabla ya alfajiri hana swawm.”[1]
Wameipokea watano. an-Nasaa´iy na at-Tirmidhiy wameegemea zaidi kwamba maneno hayo ni ya Swahabah. Ibn Khuzaymah na Ibn Hibbaan wamesahihisha Hadiyth kuwa ni maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Katika upokezi wa ad-Daaraqutwniy imekuja:
“Hana swawm yule ambaye hakulala na swawm usiku.”[2]
Hadiyth hii ni dalili inayoonyesha kuwa swawm lazima iwe na nia, kama ´ibaadah nyingine zote, jambo ambalo wanazuoni wameafikiana juu yake. Nia maana yake ni: makusudio na matakwa. Shaykh-ul-Islam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:
”Wanazuoni wameafikiana kwamba ´ibaadah zinazokusudiwa zenyewe, kama vile swalah, swawm na hijjah, haziwi sahihi isipokuwa kwa nia.”
Hii ni kwa sababu swawm ni kuacha jambo fulani ndani ya wakati maalumu. Aidha kujizuia kunaweza kuwa kwa manufaa ya kimwili. Kwa ajili hiyo swawm ikahitaji kutia nia.
Swawm inayohitaji kutia nia ni swawm ya Ramadhaan, kulipa deni la swawm ya Ramadhaan au swawm ya nadhiri, kama ilivyotajwa na at-Tirmidhi katika ”al-Jaamiy´” yake. Kuhusu swawm ya kujitolea, itakuja maelezo yake baadaye – Allaah (Ta´ala) akitaka.
Nia mahali pake ni moyoni. Kwa maana nyingine mwenye kufikiria moyoni kwamba atafunga kesho, basi amekwishanuia. Nia inasihi katika sehemu yoyote ya usiku. Hilo ni kutokana na maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“… kabla ya alfajiri.”
Kabla inajumuisha sehemu yoyote ya usiku. Hili linatiwa nguvu na riwaya ya Ibn Maajah na ad-Daaraqutwniy:
”… katika usiku.”
Miongoni mwa dalili za nia ni mfungaji kuamka kwa ajili ya daku na kujiandaa nayo, hata kama hakusimama.
[1] Ahmad (6/287), Abu Daawuud (2454), at-Tirmidhiy (730), an-Nasaa’iy (2331), Ibn Maajah (1700) na Ibn Khuzaymah (1933).
[2] ad-Daaraqutwniy (2214).
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/18-20)
- Imechapishwa: 04/02/2025

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/18-20)
Imechapishwa: 04/02/2025
https://firqatunnajia.com/13-hadiyth-yule-asiyelaza-nia-kabla-ya-alfajiri/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)