Hadiyth hii ni dalili ya kupendekezwa kuangalia mwezi mwandamo usiku tarehe thelathini wa mwezi. Hilo ni kutokana na maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Watu waliona mwezi mwandamo… ”

Khaswa kwa wale waliobarikiwa na macho makali. Inajulisha kwamba ndio ilikuwa desturi ya Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kwa sababu kuna manufaa makubwa kwa waislamu kutokana na hukumu zinazotokana na kuonekana kwake.

Hadiyth ni dalili kwamba yule mwenye kuona mwezi mwandamo anapaswa kumjulisha kiongozi au aliyeteuliwa naye kwa ajili ya kuwatangazia watu. Yeyote atakayeona mwezi mwandamo wa Ramadhaan na ushahidi wake ukakataliwa. Je, mtu ni wajibu kwake kufunga? Imeelezwa kuwa ni wajibu kwa mujibu wa wanazuoni wengi. Hilo ni kutokana na maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Fungeni kwa kuonekana kwake na fungueni kwa kuonekana kwake.”

Huyu ameuona na hivyo ni lazima afunge.”[1]

Maoni ya pili yanasema kuwa si lazima afunge, kwa sababu mwezi mwadamo ni ule unaodhihirika na kujulikana, si ule unaoonwa pekee. Hii ni maoni ya riwaya kutoka kwa Ahmad ambayo pia yamwechaguliwa na Ibn Taymiyyah[2].

Ikiwa ataona mwezi mwandamo ya Shawwaal na ushahidi wake ukakataliwa, basi asifungue. Kwa sababu mwezi mwandamo wa Shawwaal hauthibitishwi kwa mujibu wa Shari´ah isipokuwa kwa mashahidi wawili. Haya ndio maoni ya Ahmad, Abu Haniyfah na Maalik[3]. Maoni ya pili yanasema kuwa atakula kwa siri. Hayo ndio maoni ya ash-Shaafi’iy na Ibn Hazm[4]. Maoni ya kwanza ndio yenye nguvu zaidi; hatofungua kwa sababu ya kufuata kikosi kikubwa cha watu, kuchukua tahadhari katika ´ibaadah ya swawm – Allah ndiye mjuzi zaidi.

[1] al-Istidhkaar” (10/24), “al-Mughniy” (04/416), “al-Majmuu´’” (06/276), “Badaiy’-us-Swanaa’iy’” (02 /80) na “al-Mudawwanah” (01/193).

[2] al-Fataawa (25/114).

[3] Tabyiyn-ul-Haqaaiq (01/318), “Mukhtaswar-Khaliyl”, uk. 58 na “al-Mughni” (04/416).

[4] “al-Muhallaa” (06/235) na “al-Majmuu´’” (06/280).

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/17)
  • Imechapishwa: 04/02/2025