13. Hadiyth “Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimsikia bwana mmoja… “

245 – Anas (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimsikia bwana mmoja safarini mwake akisema:

الله أَكْبَرُ اللهُ أَكْبرُ

“Allaahu ni mkubwa, Allaahu ni mkubwa.”

Akasema: “Kutokana na maumbile.” Kisha bwana yule akasema:

أَشْهَدُ أَنْ لا إِله إِلا الله

“Nashuhudia ya kwamba hapana mungu wa kweli isipokuwa Allaah.”

Akasema: “Ametoka Motoni.” Watu wakamkimbilia bwana yule ambapo wakaona kuwa ni mchungaji wa kondoo ambaye ameona kuwa wakati wa swalah umekwishaingia na ndipo akaadhini.”[1]

Ameipokea Ibn Khuzaymah katika “as-Swahiyh” yake. Muslim amepokea mfano wake.

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/217)
  • Imechapishwa: 01/03/2022
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy