12. Hadiyth “Bora ya waja wa Allaah ni wale… “

244 – Ibn Abiy Awfaa (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

إن خيارَ عبادِ اللهِ الذين يراعون الشمسَ والقمرَ والنجومَ لذكرِ الله

“Bora ya waja wa Allaah ni wale wenye kuliona jua, mwezi na nyota kwa lengo la kumtaja Allaah.”[1]

Ameipokea at-Twabaraaniy na tamko ni lake, al-Bazzaar na al-Haakim ambaye amesema:

“Cheni ya wapokezi wake ni Swahiyh.”

[1] Nzuri kupitia zengine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/217)
  • Imechapishwa: 01/03/2022
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy