128. Masuala yanayohusiana na kulipiza wema kwa kafiri

Suala la pili: Kumlipa kafiri wema pale anapotufanyia wema. Si kwamba tunawapenda. Bali tunawalipa kwa kitendo chao pekee. Amesema (Ta´ala):

لَّا يَنْهَاكُمُ اللَّـهُ عَنِ الَّذِينَ لَمْ يُقَاتِلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَلَمْ يُخْرِجُوكُم مِّن دِيَارِكُمْ أَن تَبَرُّوهُمْ وَتُقْسِطُوا إِلَيْهِمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ

”Allaah hakukatazeni kuwafanyia wema na uadilifu wale wasiokupigeni vita katika dini na wala hawakukutoeni kutoka majumbani mwenu. Hakika Allaah anawapenda wafanyao uadilifu.” (al-Mumtahinah 60:08)

Ikiwa makafiri hawawapigi vita waislamu, hawawasaidii wale wanaowapiga vita na isitoshe wakawa na mkataba na waislamu, basi waislamu nao wanatakiwa kuwalipa wema kutokana na wema wao. Hili haliingii katika kujenga nao urafiki na kuwapenda, bali hili ni kwa ajili ya kulipiza wema. Uislamu unahimiza kutenda wema na kulipiza wema uliofanyiwa. Sababu nyingine ni kwamba makafiri hawabaki na huduma na deni kwa waislamu. Kulipiza wema kuna faida zake. Miongoni mwa faida zake zengine ni kuwavuta katika Uislamu. Pindi tutatangamana kwa wema pamoja na wakati huohuo wasitupige vita na wala hawawasaidii wale wanaotupiga vita. Tukitangamana nao kwa wema ni sababu inayopelekea kuingia katika Uislamu. Jengine vilevile ni kulipiza wema waliowafanyia waislamu. Tukilipiza wema waliotufanyia wanabaki hawana huduma juu yetu na sisi pia tunaweza kuwaambia ´tumewapa kama jinsi nyinyi mlivotupa` na hivyo hawana huduma ambayo wataitumia kama hoja.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 165
  • Imechapishwa: 28/02/2019