126. Waislamu hawaachi chakula chochote kwa kuona usumbufu

Chakula:

1 – ´Adiy bin Haatim (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

”Nilisema: ”Ee Mtume wa Allaah! Hakika mimi nataka kukuuliza juu ya chakula ambacho nakiacha kwa sababu ya usumbufu.” Akasema: ”Usiache kitu. Vinginevyo unawaiga manaswara[1].”[2]

[1] Kwa sababu manaswara hujizuia na aina fulani ya vyakula inapoingia katika moyo wa mmoja wao kuwa ni haramu au chenye kuchukiza. Hiyo ndio sababu ya kukatazwa. Maana yake ni kwamba usijikoseshe raha na kuona usumbufu, kwa sababu ukifanya hivo basi unajifananisha na manaswara. Hayo ni katika mambo ya manaswara na watawa wao, imekuja namna hiyo katika ”Tuhfat-ul-Ahwadhiy”.

[2] Ahmad, al-Bayhaqiy na at-Tirmidhiy kupitia kwa Shu´bah, kutoka kwa Simaak bin Harb: Nimemsikia Murayy bin Qatwariy: Nimemsikia ´Adiy bin Haatim na kadhalika. Namna hii pia ameipokea Ibn Hibbaan. Cheni hii ya wapokezi ni nzuri kupitia inayofuatia. Wapokezi wake ni wenye kuaminika na wote ni wapokezi wa Muslim – isipokuwa Murayy bin Qatwariy ambaye Ibn Hibbaan anaonelea kuwa ni mwenye kuaminika. Ibn Hajar amesema juu yake katika ”at-Taqriyb”:

”Ni mwenye kukubaliwa.”

Bi maana pale ambapo atakuwepo mwengine aliyesimulia kama yeye. Katika hali hii ameipokea Abu Daawuud, at-Tirmidhiy, Ibn Maajah, al-Bayhaqiy na Ahmad kupitia kwa Simaak bin Harb: Qabiyswah bin Hulb amenihadithia, kutoka kwa baba yake aliyesimulia kuwa amemsikia bwana mmoja akimuuliza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Kuna katika vyakula chakula ambacho nakiacha kwa kuona usumbufu?” Akasema: ”Usitilie shaka chochote. Vinginevyo unawaiga manaswara.”

Cheni hii ya wapokezi ni kama ile ilio kabla yake, isipokuwa Qabiyswah bin Hulb ambaye al-´Ijliy pia anaona kuwa ni mwenye kuaminika. at-Tirmidhiy amesema:

”Hadiyth ni nzuri.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 182
  • Imechapishwa: 13/11/2023