4 – Qadariyyah. Nao ni wale ambao wanaona kukanusha Qadar kutoka katika matendo ya mja na kwamba mja anayo matakwa na uwezo unaotoka nje ya matakwa na uwezo wa Allaah. Mtu wa kwanza ambaye alidhihirisha ´Aqiydah hiyo ni Ma´bad al-Juhaniy mwishoni mwa zama za Maswahabah. Alichukua ´Aqiydah hiyo kutoka kwa bwana mmoja mwabudia moto huko Baswrah. Wako mapote mawili; waliochupa mipaka na ambao hawachupi mipaka. Waliochupa mipaka wanapinga ujuzi, matakwa, uwezo wa Allaah na kuyaumba Kwake matendo ya mja. Aina hii wamemalizika au wanakaribia kumalizika. Aina nyingine ambayo hawakuchupa mipaka wanaamini kuwa Allaah anayajua matendo ya waja. Lakini hata hivyo wanapinga kutokea kwake kwa matakwa, uwezo na uumbaji wa Allaah. Madhehebu yao yametulizana juu ya ´Aqiydah hii.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 162
- Imechapishwa: 21/02/2023
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)