5 – Murji-ah. Nao ni wale ambao wanarejesha imani nyuma kutoka katika imani. Kwa mujibu wao matendo sio katika imani. Imani ni kule kuthibitisha kwa moyo. Kwa msemo mwingine mtenda dhambi kwa mujibu wao ni mwenye imani kamili. Haijalishi kitu yale maasi atayoyafanya au yale matendo mema atayoyaacha. Tunapomhukumu ukafiri yule ambaye anaacha baadhi ya mambo ya Shari´ah ya dini basi tumefanya hivo kwa kutotambua ndani ya moyo wake na si kwa ajili eti ameacha matendo haya. Haya ni madhehebu ya Jahmiyyah ambayo ni kinyume na madhehebu ya Khawaarij.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 163
  • Imechapishwa: 21/02/2023