6 – Mu´tazilah. Ni wafuasi wa Waaswil bin ´Atwaa´ ambaye alijitenga na kikao cha al-Hasan al-Baswriy na akathibitisha kuwa mtenda dhambi kubwa yuko katika ngazi kati ya ngazi mbili. Kwa msemo mwingine sio muumini wala kafiri. Hata hivyo atadumishwa Motoni milele. ´Amr bin ´Ubayd amemfuata katika hilo. Madhehebu yao inapokuja katika sifa za Allaah ni kukanusha kama wanavofanya Jahmiyyah. Inapokuja kunako Qadar wao ni Qadariyyah. Wanapinga mipango na Qadar ya Allaah kufungamana na matendo ya mja. Inapokuja kunako mtenda dhambi wanaona kuwa atadumishwa Motoni milele na anatoka nje ya imani na mtu huyo anakuwa katika ngazi kati ya ngazi mbili; imani na ukafiri. Wako kinyume na Jahmiyyah katika misingi hii miwili.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 163
  • Imechapishwa: 21/02/2023