124. Ndio maana Mtume alikuwa akiondoka Muzdalifah kabla ya jua kuchomoza

Hajj

1 – ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

”Washirikina walikuwa hawaondoki kwenye Mkusanyiko[1] mpaka jua lichomoze juu ya Thubiyr[2]. Walikuwa wakisema: ”Koma, ee Thubiyr, ili tuweze kuondoka zetu.” Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akajitofautisha nao na akaondoka kabla ya jua kuchomoza.”[3]

[1] Bi maana Muzdalifah. Imesemekana kuwa imeitwa Mkusanyiko kwa sababu Aadaam na Hawwaa (´alayhimaas-Salaam) wakati walipoteremshwa kutoka mbinguni walikusanyika hapo.

[2] Mlima karibu na Makkah.

[3] al-Bukhaariy, Abu Daawuud, an-Nasaa’iy, at-Tirmidhiy, ad-Daarimiy, Ibn Maajah, al-Bayhaqiy na Ahmad. at-Tirmdhiy amesema:

”Hadiyth ni nzuri na Swahiyh.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 179-180
  • Imechapishwa: 12/11/2023