120. Wakeze Mtume pia ni katika watu wa nyumbani kwake

Wakeze Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambao ndio wamama wa waumini, wanaingia ndani ya kizazi na watu wa nyumbani kwake. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema wakati alipokuwa akiwazungumzisha wakeze Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

يَا نِسَاءَ النَّبِيِّ لَسْتُنَّ كَأَحَدٍ مِّنَ النِّسَاءِ ۚ إِنِ اتَّقَيْتُنَّ فَلَا تَخْضَعْنَ بِالْقَوْلِ فَيَطْمَعَ الَّذِي فِي قَلْبِهِ مَرَضٌ وَقُلْنَ قَوْلًا مَّعْرُوفًا وَقَرْنَ فِي بُيُوتِكُنَّ وَلَا تَبَرَّجْنَ تَبَرُّجَ الْجَاهِلِيَّةِ الْأُولَىٰ ۖ وَأَقِمْنَ الصَّلَاةَ وَآتِينَ الزَّكَاةَ وَأَطِعْنَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ ۚ إِنَّمَا يُرِيدُ اللَّـهُ لِيُذْهِبَ عَنكُمُ الرِّجْسَ أَهْلَ الْبَيْتِ وَيُطَهِّرَكُمْ تَطْهِيرًا

““Enyi wake wa Nabii! Nyinyi si kama yeyote yule katika wanawake; mkiwa na taqwa, basi msilainishe kauli asije akaingiwa na tamaa yule ambaye moyoni mwake mna maradhi na semeni kauli inayokubalika. Na Tulizaneni majumbani mwenu na wala msijishauwe kwa kuonyesha mapambo kama walivyojishauwa mwanzo zama za ujahili na simamisheni swalah na toeni zakaah na mtiini Allaah na Mtume Wake. Hakika si venginevyo Allaah anataka akuondosheeni maovu, enyi watu wa nyumbani kwa Mtume, na akutakaseni mtakaso barabara.”[1]

Hata hivyo maamrisho haya yanawaelekea wanawake wote wa waumini. Wanawake wa waumini wanatakiwa kutulizana nyumbani. Wanawake wa waumini wanatakiwa kujisitiri. Ingawa hapa wanazungumzishwa wakeze Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambao ndio viigizo vyema na kama wao wameamrishwa kujisitiri, kuepuka kuonyesha mapambo na kujitia manukato wakati wa kutoka nje, watulizane nyumbani, kuswali, kutoa zakaah na kumtii Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), basi vivyo hivyo yanawahusu wanawake wote wa waumini. Kwa sababu wakeze Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndio viigizo vyema kwa wanawake wa waumini.

يَا نِسَاءَ النَّبِيِّ لَسْتُنَّ كَأَحَدٍ مِّنَ النِّسَاءِ ۚ إِنِ اتَّقَيْتُنَّ فَلَا تَخْضَعْنَ بِالْقَوْلِ فَيَطْمَعَ الَّذِي فِي قَلْبِهِ مَرَضٌ وَقُلْنَ قَوْلًا مَّعْرُوفًا وَقَرْنَ فِي بُيُوتِكُنَّ وَلَا تَبَرَّجْنَ تَبَرُّجَ الْجَاهِلِيَّةِ الْأُولَىٰ ۖ وَأَقِمْنَ الصَّلَاةَ وَآتِينَ الزَّكَاةَ وَأَطِعْنَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ ۚ إِنَّمَا يُرِيدُ اللَّـهُ لِيُذْهِبَ عَنكُمُ الرِّجْسَ أَهْلَ الْبَيْتِ وَيُطَهِّرَكُمْ تَطْهِيرًا

““Enyi wake wa Nabii! Nyinyi si kama yeyote yule katika wanawake; mkiwa na taqwa, basi msilainishe kauli asije akaingiwa na tamaa yule ambaye moyoni mwake mna maradhi na semeni kauli inayokubalika. Na Tulizaneni majumbani mwenu na wala msijishauwe kwa kuonyesha mapambo kama walivyojishauwa mwanzo zama za ujahili na simamisheni swalah na toeni zakaah na mtiini Allaah na Mtume Wake. Hakika si venginevyo Allaah anataka akuondosheeni maovu, enyi watu wa nyumbani kwa Mtume, na akutakaseni mtakaso barabara.”

Bi maana uchafu wa maasi. Ni dalili inayojulisha kwamba wakeze Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wanaingia katika watu wa nyumbani kwake. Watu wa nyumbani kwake si wale jamaa zake peke yao bali wake zake pia kwa sababu ndio wanaosemezwa hapa.

[1] 33:32-33

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 92
  • Imechapishwa: 08/09/2021