12. Yule anayemtukana mmoja katika Maswahabah

Miongoni mwa Sunnah za wazi, bainifu, zilizothibiti na zinazotambulika ni kutaja sifa nzuri za Maswahabah wote wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Sambamba na hilo inapaswa kujizuilia na mabaya yao na kunyamazia makinzano yaliyotokea kati yao.

Yeyote ambaye atamtukana yeyote katika Maswahabah wa Mtume wa Allaah, akampunguza, akamponda, akafichukua kasoro yake au aibu yake, pasi na kujali kiasi kidogo au kiasi kikubwa ambacho kinapelekea kumtukana mmoja katika wao, basi huyo ni mzushi mchafu na Raafidhwiy anayekwenda kinyume. Allaah hatokubali kutoka kwake tawbah wala fidia!

Ni Sunnah kuwapenda. Ni ´ibaadah kule kuwaombea du´aa. Ni njia kule kuwaigiliza. Ni fadhilah kuwafata.

  • Mhusika: Imaam Harb bin Ismaa´iyl al-Kirmaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Sunnah, uk. 70
  • Imechapishwa: 25/05/2022