11. Ndoto ni zenye kutoka kwa Allaah

Ndoto ni zenye kutoka kwa Allaah (´Azza wa Jall). Mwotaji akiota kitu usingizini mwake isiyokuwa mkorogano na akamsimulia ndoto yake mtu msomi ambapo mtu huyu akaifasiri kwa njia sahihi, basi kipindi hicho ndoto na tafsiri yake itakuwa ni haki. Ndoto za Mitume zilikuwa ni Wahy. Ni mjinga gani anayetukana ndoto na kudai kuwa ni upuuzi mtupu? Nimefikiwa na khabari kwamba aliyesema hivo haoni kuwa ni lazima kuoga josho la janaba baada ya kuota. Imepokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ndoto ya muumini ni mazungumzo ambayo Allaah anamzungumzisha mja Wake.”[1]

[1] Ibn ´Abiy ´Aaswim katika “as-Sunnah” (486). Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwilaal-ul-Jannah” na “Dhwa´iyf-ul-Jaami´” (3078).

  • Mhusika: Imaam Harb bin Ismaa´iyl al-Kirmaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Sunnah, uk. 69
  • Imechapishwa: 25/05/2022