10. Qur-aan ni maneno ya Allaah ambayo hayakuumbwa

Qur-aan ni maneno ya Allaah ambayo amezungumza kwayo. Haikuumbwa. Yeyote mwenye kudai kuwa Qur-aan imeumbwa ni Jahmiy na ni kafiri.

Ambaye atadai kuwa Qur-aan ni maneno ya Allaah na akachukua msimamo wa kunyamaza na akakataa kusema kuwa haikuumbwa, ni mwenye kukufuru zaidi kuliko wa kwanza. ´Aqiydah yake ni mbaya zaidi.

Ambaye atadai kuwa Qur-aan ni maneno ya Allaah lakini matamshi na kisomo chetu cha Qur-aan kimeumbwa, huyo ni Jahmiy mchafu na mzushi.

Yule ambaye hatowakufurisha watu hawa na Jahmiyyah basi yeye ni kama wao.

وَكَلَّمَ اللَّـهُ مُوسَىٰ تَكْلِيمًا

“Bila shaka Allaah alimzungumzisha Muusa maneno kikwelikweli.”[1]

Alimpa Tawraat, mkono kwa mkono. Allaah (´Azza wa Jall) daima hakuacha kuwa Mwenye kuzungumza na mtambuzi:

فَتَبَارَكَ اللَّـهُ أَحْسَنُ الْخَالِقِينَ

“Amebarikika Allaah mbora wa wenye kuumba.”[2]

[1] 4:164

[2] 23:14

  • Mhusika: Imaam Harb bin Ismaa´iyl al-Kirmaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Sunnah, uk. 64-68
  • Imechapishwa: 25/05/2022