12. Watumiaji pombe na Ramadhaan

Watenda maasi wengi wanaacha kuinywa katika zile siku tukufu, kama mfano wa Ramadhaan. Lakini wananuia kurudi kuinywa punde tu baada ya Ramadhaan kwisha. Mtu kama huyu ni chapombe na hajatubu. Jambo hili khaswa pale ambapo atakuwa ni mwenye kuhesabu siku na anasubiri tu mwezi umelizike ili aweze kurudi kutumia pombe. Kwa ajili hii unapokaribia mwezi ndio wanakunywa kwelikweli ili kuiaga kisha wakarudi kunywa punde tu baada Ramadhaan kumalizika. Baadhi yao wamesema:

Pindi kunapopita masiku ishirini ya Sha´baan

basi unywe kinywaji chako cha usiku kipindi cha mchana

Na wala usinywe kwa glasi ndogondogo

wakati umekuwa mfinyu kwa wale wachanga

Baya kuliko haya ni kwamba baadhi ya wajinga watumiaji wameyachukua maneno haya na kusema kuwa yana jumla iliyojificha ambayo haifahamiki isipokuwa tu na wale watu maalum. Kwa mujibu wao wanaona kuwa mashairi hayo yana maana kwamba mtu anatakiwa kutumia fursa ya umri wake na kumwabudu Allaah pale ambapo umekaribia muda wa kuondoka kwake. Maneno haya ni mabaya sana na yanakumbushia maneno ya shairi lingine linalosema:

Glasi ni nyembamba na pombe ni nyembamba

mambo yamefanana na ndio maana kumetokea mkanganyiko

Utasema pombe imekuwa kikombe

na utasema kikombe kimekuwa pombe

Udhahiri wa maneno haya ni dhambi tupu. Lakini baadhi ya wajinga wanadai kuwa maneno hayo yamebeba jumla iliyojificha. Hata hivyo jumla hiyo iliyojificha ni mbaya zaidi kuliko ile maana yenye kudhihiri. Kwa sababu maana ya dhahiri yake ni dhambi ilihali maana inayodaiwa kulengwa na iliyojificha ni kwamba Muumba na viumbe wamekuwa kitu kimoja mpaka yule ambaye ni mtambuzi amekuwa tena hawezi kutofautisha kati yao. Mashairi haya na mfano wake ima ni dhambi au kufuru. Si vyenginevyo hekima za kiungu zinachukuliwa kutoka katika maneno ya Allaah, maneno ya Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), maneno ya Salaf na mashairi yenye hekima.

  • Mhusika: Imaam Zayn-ud-Diyn bin Rajab al-Hanbaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Dhamm-ul-Khamr, uk. 25-26
  • Imechapishwa: 26/07/2020