Imependekezwa kuharakisha kukata swawm pale itapohakikiwa kuzama kwa jua kwa kuliona au akawa na dhana yenye nguvu kwa taarifa za mtu mwaminifu kwa njia ya adhaana au njia nyingine. Sahl bin Sa´d (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Watu hawatoacha kuwa katika kheri muda wa kuwa wanaharakisha kukata funga.”[1]

Kuna maafikiano juu yake.

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika yale aliyopokea kutoka kwa Mola Wake (´Azza wa Jall):

“Hakika waja wanaopendwa zaidi kwangu ni wale wenye kuharakisha kukata swawm.”[2]

[1] al-Bukhaariy (1957) na Muslim (49).

[2] Ahmad (12612), Abu Daawuud (2356) na at-Tirmidhi (695).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Mulakhasw al-Fiqh (01/380)
  • Imechapishwa: 30/03/2021