Wakati Imaam Maalik (Rahimahu Allaah) na wengineo katika Salaf walipoulizwa juu ya hili – namna ya sifa za Allaah – wakasema:

“Kulingana kunajulikana, namna haijulikani, kuamini hilo ni wajibu na kuuliza juu ya hilo ni Bid´ah.”[1]

Bali Yeye (Subhaanahu wa Ta´ala) ni mwenye kusifika kwa sifa, kama alivyoeleza Mwenyewe, bila ya kuzidisha wala kupunguza. Nazo ni sifa za kihakika. Kulingana ambako ni kwa hakika. Kusikia kwa hakika. Kuridhia kwa hakika. Kukasirika kwa hakika. Sifa zote hazina Majaaz. Bali ni za hakika kwa njia inayolingana na Allaah.

Hatuziwekei namna na kuzipigia mfano, hatuzishabihishi wala kuzipotosha. Bali tunazipitisha kama zilivyo dhahiri yake. Kila kilichothibiti katika andiko tunakipitisha kama kilivyokuja. Kama walivyosema Salaf:

“Zipitisheni kama zilivyokuja.”[2]

Bila ya kuzipotosha, kuzikanusha wala kuzifasiri kimakosa, Ta´wiyl. Tunazipitisha na wakati huo huo tunaamini kuwa ni za haki na kwamba ni sifa zenye kuthibiti na kwamba Allaah anasifika nazo kihakika. Tunafanya hivo bila ya kushabihisha, kufananisha, kuziwekea namna wala kuzikanusha. Namna hii ndivyo walivyosema Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah.

[1] Athar hii imepokelewa na Salaf wengi. Miongoni mwao ni Imaam Maalik, mwalimu wake Rabiy´ah bin Abiy ´Abdir-Rahmaan, Imaam ash-Shaafi´iy, al-Awzaa´iy, ath-Thawriy na wengineo.

[2] al-Khallaal katika “as-Sunnah” (01/243), al-Aajurriy katika “ash-Shariy´ah” (720), “at-Tawhiyd” (794) (03/307), al-Lalakaa´iy katika “Sharh ´Aqiydah Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah” (930) (03/527), asw-Swaabuuniy katika “´Aqiydat-us-Salaf wa Aswhaab-il-Hadiyth” (249).

  • Mfasiri: Firqatunnajia.com