Hadiyth inatiliwa nguvu vilevile na kitendo cha wanawake wengi katika wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambao walikuwa wakionyesha uso na mikono yao mbele yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pasi na yeye kuwakemea juu ya hilo. Zipo dalili nyingi juu ya hilo. Hapa tutaorodhesha baadhi ya zile ambazo nakumbuka:

2 – Ibn ´Abbaas amesimulia:

”Katika hijjah ya kuaga [siku ya kuchinja] mwanamke mmoja kutoka Khath´am alimuuliza fatwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). al-Fadhwl bin ´Abbaas, ambaye alikuwa mzuri, alikuwa ameketi nyuma yake Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akijibu maswali ya watu.

al-Fadhwl bin ´Abbaas akamgeukia[1]. Alikuwa ni mwanamke mrembo[2] na yeye pia akamtazama. Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akakishika kidevu cha al-Fadhwl na kugeuza uso wake upande mwingine.”

Kwa Ahmad al-Fadhwl mwenyewe anasimulia:

”Nikawa namtazama ambapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akanitazama na akaugeuza uso wangu mbali na uso wake. Kisha nikarudi kumtazama akageuza uso wangu mbali na uso wake. Nilifanya hivo mara tatu, sikuweza kuacha.”

Wasimulizi wake ni wenye kuaminika lakini hata hivyo cheni ya wapokezi ni yenye kukatika kwa vile al-Hakam bin ´Utaybah hakuyasikia haya kutoka kwa Ibn ´Abbaas. ´Aliy  bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kisa hichi na akasema kuwa tukio hili lilikuwa siku ya kuchinja baada ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kurusha vijiwe kwenye nguzo. Akazidisha kwa kusema:

”al-´Abbaas akamwambia: ”Ee Mtume wa Allaah! Ni kwa nini unageuza shingo ya mtoto wa ami yako?” Akajibu: ”Nimemuona kijana wa kiume na kijana wa kike na sikuweza kuwaaminisha na shaytwaan.”

[1] Katika upokezi mwingine imekuja ya kwamba alimtazama mwanamke yule na akapendezwa na urembo wake.

[2] Katika upokezi mwingine imekuja ya kwamba alikuwa mzuri.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 61-62
  • Imechapishwa: 05/09/2023