Vivyo hivyo kuhusu Hadiyth ambazo zina kujitenga; kama mfano wa Hadiyth inayosema kuwa mwenye kufanya kadhaa na kadhaa si katika sisi. Sioni chochote katika hizo kwamba maana yake ni Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kujitenga mbali au mbali na dini yake. Naonelea kuwa maana yake ni kwamba si katika wenye kututii, mwenye kutuigiliza, mwenye kuhifadhi Shari´ah yetu na kadhalika. Sufyaan bin ´Uyaynah amesema kuwa sentesi isemayo “si katika sisi” maana yake ni kwamba “si mfano wetu”. Tafsiri hiyo pia alikuwa akiwanasibishia wengine pia. Hata kama tafsiri hii ameisema imamu miongoni mwa maimamu wa elimu, mimi siikubali kwa sababu ikiwa mwenye kufanya hivo si kama Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), basi itakuwa na maana kwamba mwenye kufanya hivo anakuwa kama Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Vinginevyo hakuna tofauti kati ya mtendaji na mwachaji. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hana anayelingana naye wala mfano wake, si katika wale watendaji wala waachaji. Haya ni kuhusiana na kukanusha imani na kujitenga mbali na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kila kimoja limefungamana na kinigine. Hivo ndivo inatakiwa kufasiriwa.

  • Mhusika: Imaam Abu ´Ubayd al-Qaasim bin Sallaam
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Iymaan, uk. 85-86
  • Imechapishwa: 04/07/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naawswir-ud-Diyn al-Albaaniy