Kuhusu mapokezi yaliyopokelewa yanayosimulia maasi kama kufuru na shirki, sioni kuwa yanamthibitishia mwenye nayo ukafiri au shirki kwa njia inayomwondoshea imani mwenye nayo. Hakika hapana vyenginevyo maana yake ni kwamba ni katika tabia na mienendo ya makafiri za makafiri na washirikina. Nimepata dalili katika Qur-aan na Sunnah zinazofasiri hayo mawili ya mwanzo, kama nilivyofanya dalili kwa haya mawili ya mwisho.

Inapohusiana na shirki, Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amesema kuhusu Aadam na Hawwaa juu ya maneno ya Ibliys kwa hao wawili:

هُوَ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ وَجَعَلَ مِنْهَا زَوْجَهَا لِيَسْكُنَ إِلَيْهَا ۖ فَلَمَّا تَغَشَّاهَا حَمَلَتْ حَمْلًا خَفِيفًا فَمَرَّتْ بِهِ ۖ فَلَمَّا أَثْقَلَت دَّعَوَا اللَّـهَ رَبَّهُمَا لَئِنْ آتَيْتَنَا صَالِحًا لَّنَكُونَنَّ مِنَ الشَّاكِرِينَ  فَلَمَّا آتَاهُمَا صَالِحًا جَعَلَا لَهُ شُرَكَاءَ فِيمَا آتَاهُمَا

“Yeye ndiye aliyekuumbeni kutokana na nafsi moja na akafanya kutokana nayo mke wake ili apate utulivu. Basi anapomwingilia hubeba mimba khafifu anayotembea nayo. Kisha inapokuwa nzito humwomba Allaah Mola wao ´ukitupa mwana mwema asiyekuwa na kasoro, bila shaka tutakuwa katika wanaoshukuru`. Basi anapowapa mwana mwema asiyekuwa na kasoro, wanamjaalia washirika katika kile Alichowapa.”[1]

Kwa mujibu wa wafasiri shaytwaan aliwashawishi wampe mtoto wao jina la “´Abdul-Haarith”[2]. Je, kuna yeyote anayemtambua Allaah na dini Yake anaweza kufikiria, baada ya utume wake na nafasi yake mbele ya Allaah, kwamba waliingia ndani ya shirki? Amekiita kitendo chake kuwa ni shirki licha ya kuwa sio shirki.

[1] 7:189-190

[2] Mtunzi wa kitabu anaashiria Hadiyth:

“Wakati Hawwaa alipokuwa mjamzito, Ibliys alimtembelea. Hapo kabla hakuna yeyote katika watoto wake aliyekuwa akiishi [baada ya kuzaliwa]. Akamwambia: “Mpe jina la “´Abdul-Haarith”.” Akafanya hivo na mtoto akaishi. Hilo likawa ni katika wahy na amri ya shaytwaan.”

Hadiyth ni dhaifu, kama nilvyobainisha katika “adh-Dhwa´iyfah” (342). Dhamiri katika maneno Yake Allaah (Ta´ala):

جَعَلَا

“.. wanamjaalia… ”

Inarejea kwa mayahudi na manaswara, kama alivosema al-Hasan al-Baswriy, kama alivyopokea Ibn Jariyr kwa cheni ya wapokezi Swahiyh kutoka kwake. Hiyo ndio tafsiri bora zaidi ya Aayah hiyo, kama alivosema Haafidhw Ibn Kathiyr katika tafsiri yake.

  • Mhusika: Imaam Abu ´Ubayd al-Qaasim bin Sallaam
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Iymaan, uk. 86-88
  • Imechapishwa: 04/07/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naawswir-ud-Diyn al-Albaaniy