12. Sharti tatu za kujisafisha kwa kutumia mawe

Sharti ya kutumia mawe (الاستجمار) ni zifuatazo:

1 – Atumie mawe au kitu chengine kama mfano wa hanchifu ambacho kinaweza kusafisha maeneo hayo.

2 – Mtu asipanguse chini ya mara tatu na pia kusafike na kusibaki isipokuwa pengine ile athari ndogo isiyoondoka isipokuwa kwa maji, athari ambayo inasamehewa. Panguso moja au mbili hazitoshelezi ingawa zitasafisha maeneo hayo.

3 – Kile chenye kutoka kisizidi yale maeneo yaliyozoeleka. Hiyo ina maana kwamba endapo mkojo utaenea katika kichwa cha uume, basi haitotosha kutumia mawe bali itakuwa ni lazima kutumia maji. Vivyo hivyo endapo kilichotoka kitavuka ngiri basi haitoshelezi kujisaifisha kwa kutumia mawe. Bali ni lazima kujisafisha kwa kutumia maji.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 22-23
  • Imechapishwa: 09/12/2021