6 – Kukatika kwa yale yanayowajibisha wudhuu´

Sharti ya sita miongoni mwa sharti za kusihi kwa wudhuu´ ni kukatika kwa yale yanayowajibisha wudhuu´. Kwa mfano miongoni mwa mambo yanayowajibisha kutawadha ni kutokwa na mkojo. Wudhuu´ hausihi mpaka ukatike mkojo. Kwa mfano mtu akitawadha na huku mkojo unamtoka wudhuu´ wake hausihi. Kwa sababu hakijakatika kile kinachowajibisha. Bali ni lazima kwake kusubiri hadi kikatike kile kinachotoka nje kisha baada ya hapo ndio atawadhe. Mfano mwingine ikiwa mtu atatawadha na huku anatokwa na upepo, wudhuu´ wake hausihi. Bali anatakiwa kusubiri mpaka umalizike ule upepo unaotoka kisha baada ya hapo ndio atawadhe. Mfano wa tatu ikiwa anakula nyama ya ngamia. Katika hali hiyo anapaswa asubiri na asitawadhe mpaka atakapomaliza. Halafu baada ya hapo ndio atawadhe.

7 – Kujisafisha kwa maji au kwa kutumia mawe kabla yake

Sharti ya sita miongoni mwa sharti za kusihi kwa wudhuu´ ni kujisafisha kwa maji au kwa kutumia mawe kabla yake. Ni lazima mtu atangulize kujisafisha kwa maji au kwa mawe kabla ya kutawadha. Ima mtu ajisafishe maeneo hayo kwa kutumia maji au kwa kutumia mawe. Pindi atapotokwa na mkojo au kinyesi, basi ni lazima asafishe maeneo hayo kwa maji kabla ya kuanza kutawadha kwa njia ya kwamba aoshe ncha ya uume kwa maji na si kwamba aoshe uume wote. Anachotakiwa ni kusafisha yale pale nchani. Vivyo hivyo anatakiwa kuosha tupu ya nyuma kwa maji au kwa mawe.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 22
  • Imechapishwa: 09/12/2021