12. Dalili ya kwamba washirikina ambao Mtume aliwapiga vita walikuwa wanakiri Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Mlango wa pili

Dalili ya kwamba washirikina ambao Mtume aliwapiga vita walikuwa wanakiri Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah

Ukitaka dalili ya kwamba watu hawa ambao Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipigana nao vita walikuwa wanashuhudia hili [Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah], soma maneno Yake (Ta´ala):

قُلْ مَن يَرْزُقُكُم مِّنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ أَمَّن يَمْلِكُ السَّمْعَ وَالْأَبْصَارَ وَمَن يُخْرِجُ الْحَيَّ مِنَ الْمَيِّتِ وَيُخْرِجُ الْمَيِّتَ مِنَ الْحَيِّ وَمَن يُدَبِّرُ الْأَمْرَ ۚ فَسَيَقُولُونَ اللَّـهُ ۚ فَقُلْ أَفَلَا تَتَّقُونَ

“Sema: “Nani anayekuruzukuni kutoka mbinguni na ardhini au nani anayemiliki usikizi na uoni na nani anayemtoa aliye hai kutoka maiti, na anayemtoa maiti kutoka aliye uhai na nani anayeendesha mambo yote?” Watasema: “Ni Allaah”, basi sema: “Je, basi kwa nini hamumchi Allaah?” (10:31)

MAELEZO

Hapa mtunzi (Rahimahu Allaah) anataja dalili juu ya kwamba watu hawa walikuwa wakikubali Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah. Hata hivyo ametaja hilo kwa njia ya majibizano ili liwe na nguvu, imara na kamilifu zaidi kama dalili. Amesema:

“Ukitaka dalili ya kwamba watu hawa… ”

فَقُلْ أَفَلَا تَتَّقُونَ

“Je, basi kwa nini hamumchi Allaah?”

Hamumchi Allaah ikiwa nyinyi mnayakubali haya? Kwa vile mmethibitisha kuwa Ana umiliki mkamilifu na uendeshaji mkamilifu. Mmethibitisha kuwa Yeye peke Yake ndiye Mwenye kuumba na Mwenye kuruzuku. Mmethibitisha kuwa Yeye ndiye anamiliki kusikia na kuona kwenu. Mmethibitisha kuwa anamtoa aliye hai kutokamana na maiti na maiti kutokamana na aliye hai. Vilevile mmethibitisha kuwa Yeye ndiye anayaendesha mambo yote. Swali hili limeulizwa kama lengo la kukemea na kulazimisha. Ikiwa nyinyi mnathibitisha yote hayo, basi hilo linawalazimu kumcha Allaah na kumwabudu Yeye peke Yake hali ya yupekee hana mshirika.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Utaymiyn
  • Mfasiri: Fitqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 23
  • Imechapishwa: 23/04/2022