60 – Inatakiwa kuamini kwamba siku ya Qiyaamah kutakuwepo kulipiza kisasi kati ya viumbe wote; wanaadamu, wanyama wakali na wadudu hata sisimizi dhidi ya sisimizi nyingine. Mpaka Allaah (´Azza wa Jall) achukue haki za baadhi kutoka kwa wengine. Watu wa Peponi watapata haki zao kutoka kwa watu wa Motoni, watu wa Motoni watapata haki zao kutoka kwa watu wa Peponi, watu wa Peponi watalipana haki wenyewe kwa wenyewe, watu wa Motoni watalipana haki wenyewe kwa wenyewe.
61 – Kuyatakasa matendo kwa ajili ya Allaah.
62 – Kuridhia juu ya hukumu ya Allaah. Kuwa na subira juu ya hukumu ya Allaah. Kuamini makadirio ya Allaah yote, ya kheri na ya shari yake, matamu na machungu yake. Allaah aliyajua yale ambayo waja watayafanya na kule watakoishilia. Hawatoki ndani ya ujuzi wa Allaah. Hakukuwi kitu katika ulimwengu wala mbinguni isipokuwa kile Allaah (´Azza wa Jall) alichokijua. Tambua kwamba kile kilichokupata hakikukuwa chenye kukukosa, na kile kilichokukosa hakikuwa chenye kukupata. Hakuna muumbaji mwengine badala ya Allaah (´Azza wa Jall).
63 – Takbiyr za swalah ya jeneza ni nne. Haya ndio maoni ya Maalik bin Anas, Sufyaan ath-Thawriy, al-Hasan bin Swaalih, Ahmad bin Hanbal wanazuoni wengine wengi. Haya ndio yaliyosemwa na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
64 – Inatakiwa kuamini kuwa kila tone la mvua linaloshuka kutoka juu liko pamoja na Malaika mpaka litue pale alipoamrisha Allaah (´Azza wa Jall).
65 – Inatakiwa kuamini ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pindi alipowazungumzisha washirikina waliotupwa kisimani siku ya Badr walikuwa wakiyasikia maneno yake.
66 – Inatakiwa kuamini kuwa mtu anapokuwa mgonjwa basi Allaah anamlipa thawabu kwa maradhi hayo.
67 – Allaah anamlipa thawabu aliyekufa shahidi kwa kuuliwa kwake.
68 – Inatakiwa kuamini ya kuwa watoto wanapopatwa na kitu [cha kuumiza] hapa duniani wanaumia. Bakr bin Ukht ´Abdil-Waahid amesema eti hawaumii. Amesema uwongo.
- Mhusika: Imaam Abu Muhammad al-Hasan bin Khalaf al-Barbahaariy (kfk. 329)
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh-us-Sunnah, uk. 86-88
- Imechapishwa: 18/12/2024

Mhusika: Imaam Abu Muhammad al-Hasan bin Khalaf al-Barbahaariy (kfk. 329)
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh-us-Sunnah, uk. 86-88
Imechapishwa: 18/12/2024
https://firqatunnajia.com/12-kuwa-na-subira-juu-ya-hukumu-ya-allaah/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)