12. Je, inafaa kuwatumia wafanyakazi wasiokuwa wa kiislamu?

Swali 12: Je, inafaa kuwatumia wafanyakazi wasiokuwa wa kiislamu?

Jibu: Hapana shaka kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameamrisha kuwatoa washirikina nje ya kisiwa cha kiarabu na akaamrisha kuwatoa mayahudi na manaswara nje ya kisiwa cha kiarabu. Amesema:

“Nitawatoa mayahudi na manaswara nje ya kisiwa cha kiarabu mpaka nisimwache isipokuwa muislamu peke yake.”[1]

Hadiyth hii inajulisha kuwa mwongozo wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kwamba kisiwa cha kiarabu kusibaki isipokuwa aliye muislamu peke yake. Hilo ni kutokana na ile khatari inayopatikana kwa uwepo wa manaswara na makafiri wengine katika kisiwa cha kiarabu. Uislamu umeanza kutokea katika kisiwa hichi cha waarabu na ukaenea katika kona zote za ulimwengu. Imethibiti kwa mapokezi Swahiyh ya kwamba imani itarudi Madiynah kama ambavyo nyoka anarudi ndani ya shimo lake. Mambo yakishakuwa hivo basi itambulike kuwa kuwatumia wasiokuwa waislamu ndani ya bara hili ni jambo lina khatari kubwa, ijapokuwa hakuna khatari na madhara mengine zaidi ya kule kutangamana nao, kuwategemea na pengine hata ikatokea kumpenda. Allaah (Ta´ala) amesema:

لَّا تَجِدُ قَوْمًا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ يُوَادُّونَ مَنْ حَادَّ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَلَوْ كَانُوا آبَاءَهُمْ أَوْ أَبْنَاءَهُمْ أَوْ إِخْوَانَهُمْ أَوْ عَشِيرَتَهُمْ ۚ أُولَـٰئِكَ كَتَبَ فِي قُلُوبِهِمُ الْإِيمَانَ وَأَيَّدَهُم بِرُوحٍ مِّنْهُ

“Hutopata watu wanaomuamini Allaah na siku ya Mwisho kuwa wanawapenda wale wanaopinzana na Allaah na Mtume Wake, japo wakiwa ni baba zao, watoto wao, ndugu zao au jamaa zao. Hao [Allaah] amewaandikia katika nyoyo zao imani na akawatia nguvu kwa Roho kutoka Kwake.”[2]

Huenda akafikia kutoona tofauti ya haki na batili na hatimaye akawaona kuwa ni ndugu zetu. Pengine shaytwaan akamfanya kuwaona kuwa ni ndugu zetu katika ubinaadamu, jambo ambalo si sahihi. Udugu wa kikweli ni ule udugu wa kiimani. Hakuna udugu kwa kutofautiana kwa dini. Wakati Nuuh aliposema:

رَبِّ إِنَّ ابْنِي مِنْ أَهْلِي وَإِنَّ وَعْدَكَ الْحَقُّ وَأَنتَ أَحْكَمُ الْحَاكِمِينَ

”Ee Mola wangu! Hakika mtoto wangu ni katika ahli zangu na hakika ahadi Yako ni ya kweli Nawe ni muadilifu zaidi wa kuhukumu kuliko mahakimu wote.”[3]

Allaah akasema kumwambia:

يَا نُوحُ إِنَّهُ لَيْسَ مِنْ أَهْلِكَ

”Ee Nuuh! Hakika huyo si katika mwa ahli zako.”[4]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekata mahusiano kati ya waumini na makafiri mpaka katika kurithiana baada ya kufa. Amesema:

“Muislamu hamrithi kafiri wala kafiri hamrithi muislamu.”

Mambo yakishakuwa hivo, itambulike kuwa kuchanganyika na wasiokuwa waislamu, kuwatumia na kushirikiana nao makazini, kula, kunywa na matembezi yote haya yanapelekea kufisha ile ghera ndani ya mioyo ya waislamu mpaka anaingia ndani ya wale ambao Allaah (Ta´ala) amesema juu yao:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا عَدُوِّي وَعَدُوَّكُمْ أَوْلِيَاءَ تُلْقُونَ إِلَيْهِم بِالْمَوَدَّةِ وَقَدْ كَفَرُوا بِمَا جَاءَكُم مِّنَ الْحَقِّ

“Enyi mlioamini! Msimchukue adui Wangu na adui wenu kuwa marafiki mkiwapelekea mapenzi na hali wamekwishakanusha haki iliyokujieni.”[5]

[1] Muslim.

[2] 58:22

[3] 11:45

[4] 11:46

[5] 60:01

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: As-ilah Muhimmah, uk. 19-20
  • Imechapishwa: 01/03/2023