394 – Zayd bin Khaalid al-Juhaniy (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

مَن توضّأَ فأحسنَ وُضوءَه، ثم صلّى ركعتين، لا يسهو فيهما؛ غُفِر له ما تقدَّم من ذنبه

“Yule ambaye atatawadha na akafanya vizuri wudhuu´ wake, kisha akaswali Rak´ah mbili bila kuwazana sana, isipokuwa atasamehewa madhambi yake yaliyotangulia.”[1]

Ameipokea Abu Daawuud. Upokezi wake mwingine unasema:

ما من أحدٍ يتوضأُ فَيُحسنُ الوضوءَ، ويصلي ركعتين يُقبِلُ بقلبِه وبوجهه عليهما؛ إلاَّ وجَبَتْ له الجنةُ

“Hakuna mja yeyote atakayetawadha na akafanya vizuri wudhuu´, na akaswali Rak´ah mbili na akaielekezea moyo na uso wake wote, isipokuwa itamthubutukia Pepo.”

[1] Nzuri na Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/282)
  • Imechapishwa: 02/12/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy