Mazishi

1 – Jaabir bin ´Abdillaah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Tunazika kwenye mwanandani na watu wa Kitabu wanazika moja kwa moja kwenye shimo.”[1]

[1] at-Twahaawiy katika ”Mushkil-ul-Aathaar”, Ahmad, Ibn Sa´d na wengineo. Imepokelewa pia kutoka kwa ´Abbaas. Nimezungumzia njia zake na kubainisha yaliyosemwa juu yake katika ”Naqdu Kitaab-it-Taaj” (299). Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

”Imepokelewa kupitia njia nyingi ambazo ni zenye ulaini. Lakini zinasadikishana. Hadiyth inazindua kuwa tunatakiwa kujifautisha na watu wa Kitabu hata katika jambo la kumuweka maiti ndani ya kaburi.” (Iqtidhwaa’-us-Swiraat al-Mustaqiym, uk. 33)

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 175-176
  • Imechapishwa: 06/11/2023