115. Msifanye kama wanavofanya wafursi na warumi

6 – Jaabir bin ´Abdillaah (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

”Wakati Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipougua tuliswali nyuma yake hali ya kuwa amekaa. Abu Bakr akiwasikilizisha watu Takbiyr yake. Akatugeukia akatuona tumesimama. Akatuashiria tukaketi chini. Tukaswali nyuma yake kwa kukaa. Alipomaliza kuswali, akasema: ”Mmekaribia kufanya kama wanavofanya wafursi na warumi pindi wanaposimama kwa ajili ya wafalme wao hali ya kuwa wameketi chini. Msifanye hivo. Wafuateni maimamu wenu. Wakiswali kwa kusimama, basi nanyi swalini kwa kusimama, na wakiswali kwa kukaa chini, basi nanyi swalini kwa kukaa chini.”

Imekuja katika upokezi mwingine:

”Msifanye kama wanavofanya wafursi kwa wakuu wao.”[1]

[1] Muslim na Abu ´Awaanah. Hadiyth imepokelewa kwa mapokezi mengi kutoka kwa Jaabir. Tumeipokea kupitia njia tatu kutoka kwake, na tumezitaja katika ”Swahiyh Sunan Abiy Daawuud” (615) na (619) na ”Swifatu Swalaat-in-Nabiy”. Ziada ya mwisho wake iko kwa Abu Daawuud na wengineo kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 173-174
  • Imechapishwa: 05/11/2023