5 – ´Abdullaah bin ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Akiswali mmoja wenu ndani ya nguo moja, basi aifunge kiunoni mwake. Asivae ovyo ovyo kama mayahudi.”[1]

[1] al-Bayhaqiy na at-Twahaawiy kwa cheni ya wapokezi Swahiyh. Nimetaja mfano wake katika ”Swahiyh Sunan Abiy Daawuud” (645). Naonelea kuwa maoni sahihi zaidi ni kwamba Hadiyth ni maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ingawa msimulizi wake wakati mwingine anasitasita. Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

”Maana hii imepokelewa sahihi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kupitia kwa Jaabir na wengineo, kwamba anayeswali ndani ya nguo yenye kubana basi aikaze kiunoni na asiiache. Haya ndio maoni ya kikosi kikubwa cha wanazuoni… Maneno yake kusema ”Asivae ovyo ovyo kama mayahudi” ni nyongeza ya kuonyesha kuwa kitendo hicho kimekatazwa, kama tulivyotangulia kuzindua jambo hilo.” (Iqtidhwaa’-us-Swiraat al-Mustaqiym, uk. 42)

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 172-173
  • Imechapishwa: 05/11/2023