114. ´Aqiydah ya Sufyaan ath-Thawriy

Sufyaan ath-Thawriy (97-161), mwanachuoni wa zama zake.

126 – Kuna watu kadhaa ambao wamepokea kutoka kwa Ma´daan, ambaye kwa mujibu wa Ibn-ul-Mubaarak ni kwamba alikuwa ni mmoja katika ´Abdaal[1], aliyesema:

”Nilimuuliza Sufyaan ath-Thawriy kuhusu maneno Yake (Ta´ala):

وَهُوَ مَعَكُمْ أَيْنَ مَا كُنتُمْ ٌ

”Naye Yu pamoja nanyi popote mlipo.”[2]

Akajibu:

”Bi maana kwa ujuzi Wake.”[3]

al-Waliyd amesimulia kwamba amesema kuhusu Hadiyth za sifa:

”Zipitisheni kama zilivyokuja.”

127 – al-Layth bin Yahyaa al-Bukhaariy amesema: Ibraahiym bin al-Ash´ath amenihadithia, kutoka kwa Mu-ammal bin Ismaa´iyl, kutoka kwa Sufyaan ath-Thawriy, ambaye amesema:

”Yule mwenye kusema kuwa Qur-aan ni kiumbe ni kafiri.”[4]

Imamu huyu ambaye hakuna na kifani kabisa katika zama zake alisimulia Hadiyth nyingi kuhusu sifa. ´Aqiydah yake ilikuwa kuzithibitisha na kuzipitisha na kukomeka na kuzipindisha maana – Allaah amrehemu!

128 – Shu´ayb bin Harb amesema:

”Nilisema kumwambia Sufyaan: ”Nisimulie kitu kuhusiana na ´Aqiydah.” Akasema: ”Qur-aan ni maneno ya Allaah. Haikuumbwa. Imeanza kutokea Kwake na Kwake ndio itarejea. Yeyote mwenye kusema kinyume na haya ni kafiri. Imani ni maneno na vitendo. Inazidi na kushuka… ”Akataja mambo mengi.”

[1] Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:

”Hawa ni wale wenye kubadilishana baadhi kwa wengine. ´Abdaal ni wanachuoni ambao hawa wanawarithi wengine. Kwa maana ya kwamba anapokufa mwanachuoni huyu anakuja baada yake mwengine mpaka kifike Qiyaamah.” (Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah).

[2] 57:4

[3] Ahmad bin ´Abdillaah katika “as-Sunnah”, uk. 72, al-Aajurriy (289) na al-Laalakaa’iy (1/92/2). Ma´daan huyu simjui alikuwa ni nani. Kwa al-Bayhaqiy ameelezwa kuwa ni mfanya ´ibaadah – na Allaah ndiye mjuzi zaidi. Kwa al-Aajurriy amekuja kama Khaalid bin Ma´daan, jambo ambalo ni kosa la uchapishaji kwani huyu Khaalid bin Ma´daan alikuwa ni mwanafunzi wa Maswahabah. Mtunzi amesema katika ufupisho wake kwamba ”masimulizi haya yamethibiti kutoka kwa Ma´daan”.

[4] Sikumpata wasifu wa huyu al-Layth bin Yahyaa al-Bukhaariy. Mu-ammal bin Ismaa´iyl alikuwa ni mkweli na alikuwa na kumbukumbu mbaya. Ibraahiym alikuwa ni madhubuti kwa mujibu wa Ibn Hibbaan na al-Haakim, ilihali Abu Haatim amemsema vibaya.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 137-138
  • Imechapishwa: 17/07/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy