Abu Muhammad ´Abdullaah bin Abiy Zayd al-Qayrawaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:

Bora ya Maswahabah ni wale makhaliyfah waongofu na wenye kuongoza Abu Bakr, ´Umar, ´Uthmaan na kisha ´Aliy – Allaah awe radhi nao.

MAELEZO

Utukufu wa Maswahabah unatofautiana. Licha ya fadhilah zao zilizoenea na walizopwekeka nazo kutokamana na Ummah, wanashindana wao kwa wao. Wabora wao ni wale makhaliyfah waongofu na wenye kuongoza Abu Bakr, ´Umar, ´Uthmaan na kisha ´Aliy – Allaah awe radhi nao wote. Mpangilio wao katika fadhilah ndivo ulivyo mpangilio wao katika ukhaliyfah.

Kisha wale wengine kumi waliobaki ambao wameahidiwa Pepo: Twalhah, az-Zubayr, ´Abdur-Rahmaan bin ´Awf, Sa´d bin Abiy Waqqaas, Sa´iyd bin Zayd bin al-Khattwaab (mtoto wa ami yake ´Umar bin al-Khattwaab) na Abu ´Ubaydah bin al-Jarraah. Hawa ndio wale kumi walioahidiwa Pepo.

Kisha wanafuatia wale Maswahabah walioshiriki vita vya Badr na halafu wale Maswahabah waliokula kiapo chini ya mti. Isitoshe Wahajiri ni bora kuliko Wanusuraji. Kisha wanafuatia wale Maswahabah walioingia katika Uislamu kabla ya Ufunguzi na kisha mwishowe ni wale Maswahabah walioingia katika Uislamu baada ya Ufunguzi. Hawa wote ni Maswahabah, lakini wanatofautiana kati yao – Allaah awe radhi nao nao wawe radhi Naye!

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 82-83
  • Imechapishwa: 02/09/2021