11. Sababu ya saba ya talaka ambayo ni kung´ang´ania mume ampe talaka

07 – Mke kumuomba na kumg´ang´ania mume amwache

Anamuomba mume wake talaka wakati anapoingia na wakati anapotoka. Masikini huyu hajui kuwa ameingia katika dhambi kubwa asipokuwa na sababu inayokubalika kwa mujibu wa Shari´ah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ametahadharisha jambo hilo na akawatishia Maswahabah zake. Thawbaan (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Mwanamke yeyote ambaye anamuomba mume wake talaka pasi na sababu, basi ni haramu kwake harufu ya Pepo.”[1]

Ameipokea Ibn Maajah na ni Hadiyth Swahiyh.

Vilevile Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Mwanamke hamuombi mume wake talaka pasi na neno ambapo akapata harufu ya Pepo. Hakika Pepo yake inapatikana mwendo wa miaka arobaini.”[2]

Ameipokea Ibn Maajah (2054).

Kwa hivyo mwanamke anayemuomba mume wake talaka yuko katika khatari kubwa.

[1] Ibn Maajah (2055). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”al-Irwaa´” (2036).

[2] Ibn Maajah (2054). Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Dhwa´iyf Ibn Maajah” (445).

  • Mhusika: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Twalaaq – asbaabuhu wa ´ilaajuh, uk. 26-27
  • Imechapishwa: 04/04/2024