Miongoni mwa sababu za kufanya familia kuwa na furaha ni mume na mke kujengeana dhana nzuri. Mume aingie katika nyumba ya ujumba ilihali anamdhania vizuri mke wake kuanzia katika namna ya kutangamana naye na tabia yake. Mke akifanya jambo na akakosea basi alifasiri kwa dhana nzuri, ampe udhuru na alichukulie vizuri. Endapo atapitiliza na akashindwa kumchukulia na kumdhania vizuri, basi aone kuwa ni kosa lililotokamana na mwenye busara. Hivyo atakuwa hakumchukulia.

Kadhalika mke anatakiwa kumjengea dhana nzuri mume wake na ayafasiri mambo kwa namna iliokuwa nzuri. Kila mmoja katika wao asamehe kuteleza kwa mwengine. Hii ni miongoni mwa tabia kubwa ya mwanaume na mwanamke.

  • Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliymillaah ar-Ruhayliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Asbaab sa´aadat-il-Usrah, uk. 39-40
  • Imechapishwa: 09/10/2016