11. Mizozo iliokuwa kati ya Mitume na watu wao

Ukishahakikisha ya kwamba walikuwa wanakubali hili, lakini hili halikuwaingiza katika Tawhiyd ambayo aliwalingania kwayo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), na ukajua ya kwamba Tawhiyd waliyoipinga ni Tawhiyd-ul-´Ibaadah ambayo washirikina katika zama zetu wanaiita “al-I´itiqaad”,

MAELEZO

Ukishatambua kuwa washirikina walikuwa wakikubali Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah na walichokuwa wakikanusha ni Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah na kwamba walikuwa wakisema kuwa Allaah ndiye Muumbaji, Mruzukaji, Muhuishaji na Mfishaji. Lakini pamoja na yote haya wanapoambiwa waseme ´hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah` wanasema:

أَجَعَلَ الْآلِهَةَ إِلَـٰهًا وَاحِدًا ۖ إِنَّ هَـٰذَا لَشَيْءٌ عُجَابٌ

“Amewafanya waungu wote kuwa ni mungu Mmoja? Hakika hili ni jambo la ajabu mno.” (38:05)

Bi maana wanapoambiwa wamuabudu Allaah Mmoja asiyekuwa na mshirika wanasema kama walivyosema watu wa Nuuh kabla yao:

لَا تَذَرُنَّ آلِهَتَكُمْ وَلَا تَذَرُنَّ وَدًّا وَلَا سُوَاعًا وَلَا يَغُوثَ وَيَعُوقَ وَنَسْرًا

“Msiwaache miungu yenu na wala msimwache Wadd, wala Suwaa´, wala Yaghuuth, Ya’uuq na Nasr.” (71:23)

Kadhalika washirikina hawa mzozo uliokuwa baina yao na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ilikuwa ni katika kumuabudu Allaah Mmoja asiyekuwa na mshirika. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiwaambia:

“Semeni ´hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah` mtaokoka.”” Ahmad (03/492).

Nao wanasema:

أَجَعَلَ الْآلِهَةَ إِلَـٰهًا وَاحِدًا

“Amewafanya waungu wote kuwa ni mungu Mmoja?” (38:05)

Walikuwa wanasema kuwa hiyo ndio dini ya mababa zao na mababu zao. Pindi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipomuomba Abu Twaalib alipokuwa katika kukata roho aseme “hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah” alikataa kusema hivo na hatimaye akasema:

“Mimi niko katika dini ya ´Abdul-Muttwalib.” Al-Bukhaariy (1294), Muslim (24), an-Nasaa´iy (2035) na Ahmad (05/433).

Dini ya ´Abdul-Muttwalib ilikuwa ni kuabudu masanamu. Huu ndio ulikuwa mzozo baina ya Mitume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam) na watu wao. Mitume walikuwa wakiwaambia watu wao wamwabudu Allaah na wala wasimshirikishe na chochote. Lakini hata hivyo washirikina hawataki jengine isipokuwa kuendelea kuyaabudu makaburi. Magomvi yaliyokuwa kati ya Mitume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam) na watu wao ilikuwa ni katika Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah. Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah ilikuwa ni maafikiano kwa watu wote. Hawakuzozana nayo. Walienda kinyume katika Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah ndio ambayo ilikuwa sehemu ya mgogoro. Ndio ambayo Jihaad katika njia ya Allaah imewekwa kwa ajili yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Nimeamrishwa niwapige watu vita mpaka washuhudie ´hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah`.” al-Bukhaariy (385), at-Tirmidhiy (2608), an-Nasaa´iy (3967), Abu Daawuud (2641) na Ahmad (03/225).

Katika upokezi mwingine imekuja:

“…. katika washuhudie ´hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah`.” al-Bukhaariy (25) na Muslim (22).

Lau Mitume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam) wangeliwataka wakubali Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah basi kusingelikuwa kati yao magomvi yoyote kwa kuwa ni kitu ambacho walikuwa wakikitambua.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 22-23
  • Imechapishwa: 08/10/2016