393 – Yuusuf bin ´Abdillaah bin Salaam ameeleza:
“Nilimwendea Abud-Dardaa´ katika maradhi yake aliyofariki kwayo. Akasema: “Ee mtoto wa ndugu yangu kipenzi! Ni kipi kilichokufanya ukaja katika mji huu?” Nikasema: “Hakuna kingine isipokuwa mahusiano yaliyokuwa kati yako na baba yangu ´Abdullaah bin Salaam.” Akasema: “Ni uwongo mbaya uliyoje huu. Nimemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:
من توضّأَ فأحسنَ الوضوءَ، ثم قام فصلّى ركعتين (أو أربعاً، يشك سهل) يُحسن فيهن الذِّكْر والخشوعَ، ثم يستغفرُ اللهَ؛ غُفِرَ له
“Yule atakayetawadha na akafanya vizuri wudhuu´, kisha akasimama na kuswali Rak´ah mbili – au nne, Sahl ametia shaka – ambazo akafanya vizuri Dhikr na unyenyekevu ndani yake halafu akamuomba msamaha Allaah, basi Allaah atamsamehe.”[1]
Ameipokea Ahmad kwa cheni ya wapokezi nzuri.
[1] Nzuri.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/281-282)
- Imechapishwa: 01/12/2023
- Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)