11. Hadiyth ”Sikuchukizwa na jambo lolote, isipokuwa tu… ”

26 – Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa alipofika Madiynah aliambiwa:

”Ni kipi kinachokuchukiza juu yetu tangu siku ulipoachana na Mtume wa Allaah?” Akasema: ”Sikuchukizwa na jambo lolote, isipokuwa tu ninyi hampangi sawa safu zenu.”[1]

27 – Abu Bakrah Nufay’ bin al-Haarith ath-Thaqafiy ameeleza ya kwamba alifika kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hali ya kuwa yeye amerukuu ambapo na yeye akarukuu kabla ya kufika katika safu. Akamweleza hayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye alimwambia:

”Allaah akuzidishie bidii, lakini usirudie tena.”[2]

Shaykh Ibn Baz (Rahimahu Allaah) amesema:

”Ni wajibu kwa waislamu ni kusawazisha safu, kuziba mapengo kwa kukaribiana na kuunganishwa mguu kwa mguu pasi na kuwadhuru wengine. Ni wajibu kwa imamu kuwazindua juu ya hilo, kuwaamuru kusawazisha safu na kuzijaza kwa ukamilifu… Ni wajibu kwa kila muislamu lazima kuwachunga wale waliomzunguka ili wote waweze kushirikiana katika kupanga sawa safu na kuziba mapengo.”[3]

Mwisho.  Namuomba Allaah, Aliye juu na Mtukufu, ainusuru dini Yake, alifanye neno Lake kuwa juu, aithibitishe haki, aisambatatishe batili, awanusuru wale wenye kumtii na awadhalilishe wale wenye kumuasi. Vilevile tunamuomba aturuzuku elimu yenye manufaa, matendo mema, kuwa imara juu ya Qur-aan na Sunnah na kwa mujibu wa ufahamu wa Salaf.

Swalah  na amani ziwe juu ya Mtume wetu Muhammad, familia yake na Maswahabah zake.

al-Hudaydah –Masjid-us-Sunnah.

10/01/1428

Abu Ibraahiym

[1] al-Bukhaariy (691).

[2] al-Bukhaariy (750), Abu Daawuud (683) na an-Nasaa’iy “as-Sughraa” (2/188) na katika “al-Kubraa” (854) na Ahmad (5/46,45,39) toleo la zamani.

al-Bukhaariy ameifanyia kichwa cha khabari kinachosema ”Mlango unaohusu ambaye anarukuu kabla ya kufika katika safu.”

[3] Majmuu´-ul-Fataawaa (12/200-201).

  • Muhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wasswaabiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ujuwb Taswiyat-is-Sufuuf
  • Imechapishwa: 03/02/2025