11. Fatwa juu ya Salmaan al-´Awdah na Safar al-Hawaaliy ni za uongo?

Swali 11: Baadhi ya vijana wanatilia shaka usahihi wa fatwa iliyotolewa kwa mnasaba wa Salmaan al-´Awdah na Safar al-Hawaliy na wanasema kuwa baraza la Kibaar-ul-´Ulamaa´ haikuzungumza namna hiyo na kwamba ni jambo wamezuliwa uongo na serikali. Je, madai haya ni sahihi?

Jibu: Madai haya yaliyozuliwa yanatoka kwa viongozi wa Hizbiyyuun. Vinginevyo wanaweza siku zote kwenda kwa Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz na kumuuliza kuhusu hilo au wakamuandikia mmoja katika wanachama wa baraza la wanachuoni wakubwa na kumuuliza. Si wapo jameni.

Hizbiyyuun wanachotaka kwa yote haya ni kuitukana nchi. Wanachotaka ni kusema nchi inataka kuwafunga wanachuoni bila ya kosa lolote, jambo ambalo ni uongo. Nchi ni adilifu na himdi zote ni za Allaah. Nchi haikuwafunga kwa sababu ya yale yanayosemwa juu yao. Nchi iliwafunga baada Kibaar-ul-´Ulamaa´ kujadiliana nao kwanza na kuwataka wajirudi kwa yale waliyosema na kufanya. Wakakataa. Ndipo Kibaar-ul-´Ulamaa´ wakaamua wabaki katika hali waliyomo na wakawakataza kuzungumza ili kuilinda jamii. Hii hapa fatwa. Wanaosema namna hii wanaitukana nchi na kuwatukana Kibaar-ul-´Ulamaa´. Haijuzu.

Lau haya yangelikuwa ni manasibisho ya uongo kwa Kibaar-ul-´Ulamaa´ basi wanachuoni wasingeweza kuyanyamazia na khaswa  kwa kuzingatia ya kwamba yanatoka kwa Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz ambaye anazungumza kwa jina la wanachama wa baraza wote na inapigwa muhuri wake kutoka kwa waziri wa mambo ya ndani.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fataawaa al-Jaliyyah
  • Imechapishwa: 16/07/2017