10. Unasemaje kwa wale wenye kuchana vitabu vya Ruduud?

Swali 10: Unasemaje kwa wale ambao wamechana kitabu “al-Qutwbiyyah”, “Madaarik-un-Nadhwar” na “al-Irhaab” kutokana na madai yaliyotangulia?”

Jibu: Kuchana vitabu ambavyo vinaibainisha haki na kuamrisha kuifuata, vinaiponda batili na kuamrisha kujiepusha nayo, mwenye kufanya hivo anaingia katika wale ambao wanazuia na njia ya Allaah (´Azza wa Jall). Hakika Allaah atamuuliza juu ya kitendo hichi pale ataposimama mbele Yake hali ya kuwa hana kitu zaidi ima kheri au shari alioitanguliza. Hiki ni kitendo cha watu wa batili na wapotevu. Watu hawa wanataka kufanya vitabu vitu ni kama “Shams-ul-Ma´aarif” na vyenginevyo katika vitabu vya uchawi. Sivyo hivyo. Haya ni maneno na madai batili. Ni wajibu kwa mwenye kusema hivi amche Allaah na atambue kuwa kwa kitendo chake hichi anazuia [watu] na njia ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Huyu ni mwenye kueneza ufisadi katika ardhi. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:

وَلَا تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ بَعْدَ إِصْلَاحِهَا

“Na wala msifanye ufisadi katika ardhi baada ya kutengenea kwake.”[1]

إِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ الْمُفْسِدِينَ

“Hakika Allaah hapendi mafisadi.”[2]

[1] 07:56

[2] 28:77

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fataawaa al-Jaliyyah
  • Imechapishwa: 16/07/2017