11. Dalili ya kwamba Allaah yuko juu ya mbingu

11- ´Umar bin Ibraahiym bin Ismaa´iyl al-Imaam ametuhadithia: Ja´far bin Ma´aaliy ametuhadithia: `Umar bin Haaruun ametuhadithia: Abuu Kurayb ametuhadithia: Abuu Mu´aawiyah ametuhadithia, kutoka kwa Sa´iyd bin Marzabaan, kutoka kwa ´Ikrimah, kutoka kwa Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anh) aliyesema:

“Kuna mwanaume alikuja kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiwa pamoja naye mwanamke asiyekuwa mwarabu mweusi na kusema: “Nalazimika kumwacha mtumwa huru. Huyu atafaa?” Akamuuliza (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Allaah yuko wapi?” Akaashiria kwa mkono wake juu mbinguni. Akamuuliza: “Mimi ni nani?” Akasema: “Wewe ni Mtume wa Allaah.” Ndipo Mtume akasema: “Mwache huru. Hakika ni muumini.”

Hadiyth ya Mu´aawiyah bin al-Hakam ina mlolongo wa wapokezi ulio Swahiyh zaidi kuliko hii[1].

[1] Muslim (37).

  • Mhusika: Imaam Abu Ismaa´iyl ´Abdullaah bin Muhammad al-Answaariy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Arba´uun fiy Dalaa-il-it-Tawhiyd, uk. 33
  • Imechapishwa: 15/01/2017