109. Radd juu ya uongo wa Ibn Suwhaym kwamba Shaykh anataka kubomoa kuba la Mtume

Maneno yake:

“Na kwamba eti nasema laiti lingeweza kubomoa kuba la Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) basi ningefanya hivo.”

Hii ni moja katika uongo juu ya Shaykh. Kwa sababu ni jambo linalotambulika kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amezikwa kwenye nyumba yake hali ya kuwa ni mwenye kuhifadhiwa kutokamana na uchupaji mpaka. Nyumba yake iko na kuta na paa. Paa ilikuweko tokea kipindi azikwe (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kubwa lililofanywa ni kwamba paa iliondoshwa na ikafanywa kwa aina ya kuba. Shaykh haoni kuwa hilo ni kosa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alizikwa nyumbani kwake na akaendelea (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hali ya kuwa ni mwenye kuzikwa nyumbani kwake akiwa ni mwenye kulindwa kutokamana uchupaji mpaka. Hayo yamesemwa na ´Aaishah wakati alipotaja makatazo ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya kuchupa mpaka kwenye makaburi:

“Lau isingelikuwa ni jambo hilo basi lingeliacha waziwazi kaburi lake. Lakini alichelea lisifanywe ni mahali pa kuswalia.”[1]

Ndipo akazikwa nyumbani kwake kwa ajili ya kumlinda kutokamana na uchupaji mpaka. Wakamtuhumu Shaykh. Wanafanya kuba la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kama makuba mengine yaliyo juu ya makaburi yaliyojengewa kwa ajili ya kuyaadhimisha jambo ambalio ni kosa. Makuba yaliyojengwa juu ya makaburi ni kwenda kinyume na Shari´ah. Tunachomaanisha ni maiti akazikwa na juu ya kaburi lake kukawekwa jengo na kuba au kukafanywa ni mahali pa kuswalia. Haya ndio mambo ambayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza. Kwani ni njia inayopelekea katika shirki. Maswahabah, ambao ndio watu wabora katika Ummah, walikuwa wakizikwa al-Baqiy´. Juu ya makaburi yao hakuwekwi kitu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwekwa ndani ya nyumba yake kwa ajili ya kumlinda kutokamana na uchupaji mpaka. Kuna tofauti kati ya kaburi lililojengewa kwa ajili ya kulichupia mpaka na aliyezikwa nyumbani kwake kwa ajili ya kumlinda kutokamana na uchupaji mpaka.

Kulijengea kaburi kwa ajili ya kuliadhimisha ni jambo limekatazwa. Jengine ni njia moja wapo inayolekea katika shirki. Isitoshe ni jambo linawafanya wale wasiokuwa na elimu kufungamana nalo. Lakini kaburi la Mtume halikujengewa. Alizikwa nyumbani kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) tu. Tumejua sababu; kwa ajili ya kumlinda.

Mnasemaje endapo Mtume angezikwa al-Baqiy´? Kungekuwa msongamano, uchupaji mpaka kiasi gani na matendo ya wajinga? Lakini Allaah akamwitikia du´aa ya Mtume Wake pale aliposema:

“Ee Allaah! Nakuomba usilifanye kaburi langu kuwa ni sanamu lenye kuabudiwa.”[2]

Allaah akamwitikia du´aa yake ambapo akazikwa nyumbani kwake kwa ajili ya kumlinda. Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema:

Mola wa walimwengu akamwitikia du´aa yake Akamzungushia kuta tatu[3]

Hii ndio tofauti kati ya kaburi la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na ya wengineo yaliyojengewa. Mtu asitatizwe na hayo mawili na tukasemma kuwa kaburi la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) limejengewa na juu yake kuna kuba. Kujengea juu ya hayo inafaa kujenga juu ya makaburi mengine na kuyawekea makuba. Hivo ndivo wanavosema makhurafi.

[1] al-Bukhaariy (1330) na Muslim (529) kupitia kwa ´Aiashah (Radhiya Allaahu ´anhaa).

[2] Maalik katika ”al-Mutwattwa´” (414) mursal kutoka katika Hadiyth ya ´Atwaa´ bin Yasaar (Radhiya Allaahu ´anh). Vilevile amepokea Imaam Ahmad katika ”al-Musnad” (02/246 nambari. 7358) mfano wake na wengineo.

[3] Tazama ”Sharh-un-Nuuniyyah” (02/352) ya Ahmad ´Iysaa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-il-Imaam Mujaddid Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab, uk. 151-152
  • Imechapishwa: 08/06/2021