108. Radd juu ya uongo wa Ibn Suwhaym kwamba Shaykh ni anawakufurisha wafanyao Tawassul

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Kwamba eti mimi namkufurisha anayefanya Tawassul kwa waja wema na kwamba eti mimi namkufurisha al-Buuswayriy pale aliposema:

Ee kiumbe mbora!

Na kwamba eti nasema laiti lingeweza kubomoa kuba la Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) basi ningefanya hivo.

MAELEZO

Kwamba eti mimi namkufurisha anayefanya Tawassul… – Kuhukumu hivi moja kwa moja si sahihi. Kuna upambanuzi juu ya jambo la Tawassul. Ikiwa anamtekelezea kitu katika ´ibaadah yule anayemfanyia Tawassul, kama wafanyavo waabudia makaburi ambao wanawaendea wafu, wanawawekea nadhiri na kuwataka uokozi, hii ni shirki kubwa. Kwa sababu ni kumwabudu mwengine asiyekuwa Allaah. Ama ikiwa hamfanyii kitu katika ´ibaadah, bali anachofanya ni kwamba anawafanya Tawassul kwa Allaah kupitia wao kitendo hicho ni cha kizushi na sio ukafiri. Kwa mfano kuomba kwa jaha, kwa haki ya fulani, kwa Mtume Wake au kwa mja Wake fulani pasi na kumtekelezea mtu huyo chochote katika ´ibaadah. Alichofanya kuwajaalia wakatikati baina yake yeye na Allaah katika kumkubalia maombi yake. Hii ni Bid´ah. Kwa sababu Allaah ametuamrisha kumwomba Yeye bila kuweka mkatikati baina yetu sisi na Yeye.

Kwa hiyo kusema kwao kwamba Shaykh anakufurisha kwa Tawassul moja kwa moja hivi ni uongo. Shaykh ni mwenye kupambanua katika jambo hili.

Maneno yake:

“Eti mimi namkufurisha al-Buuswayriy pale aliposema:

Ee kiumbe mbora!

Haya ni masuala ya kumkufurisha mtu kwa kumlenga. Ni kama kwamba Shaykh haoni kumkufurisha mtu kwa dhati yake. al-Buuswayriy maneno yake ni kufuru. Amesema pindi alipokuwa akimsemeza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

Ee kiumbe mbora! Sina mwengine zaidi yako
wa kumkimbilia wakati wa majanga

Usiponitukuza siku ya Qiyaamah na
ukanishika mkono, nimeangamia.

Katika ukarimu wako ni pamoja na dunia hii
na mali zake

na miongoni mwa elimu zako ni pamoja na
elimu na Ubao na Kalamu…[1]

Hii ni kufuru. Lakini huenda mtu hakufikiwa na hoja au akawa ni mwenye kupindisha maana. Kwa hiyo hakufurishwi mpaka kwanza asimamishiwe hoja. Jengine ni kwamba hajui alikufa akiwa na hali gani.

[1] Tazama ”ad-Durar as-Saniyyah” (11/132) na yaliyo baada yake na (11/222) na yaliyo baada yake na (11/229) na yaliyo baada yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-il-Imaam Mujaddid Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab, uk. 150-151
  • Imechapishwa: 07/06/2021