Swali: Jambo la kuwafutarisha wafungaji hufanyika kwa wingi ndani ya Ramadhaan na khaswa wafanyakazi. Tatizo ni kwamba baadhi yao hawaswali au hawahudhurii swalah ya mkusanyiko licha ya kuwa msikiti uko karibu nao. Je, ni sahihi kuwafutarisha watu kama hawa?

Jibu: Kinachozingatiwa ni wale watu wengi wanaofutari. Ikiwa wengi wao ni wale wanaohifadhi swalah, basi hakutozingatiwa wale walio pamoja nao ambao hawahifadhi swalah. Jengine pia ni kwamba pengine katika kufanya hivo kukawafanya kutubia.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://ar.islamway.net/fatwa/59323/
  • Imechapishwa: 26/03/2022