106. Radd juu ya uongo wa Ibn Suwhaym kwamba Shaykh anadai Ijtihaad

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Kwamba mimi nadai Ijtihaad na kwamba mimi nimetoka nje ya Taqliyd.

MAELEZO

Kwamba mimi nadai Ijtihaad – Wanasema juu yake kwamba anadai kwamba ni mwenye kujitegemea katika Ijtihaad na kwamba anakinzana na wale maimamu wanne. Huu ni uongo. Shaykh ni Hanbaliy. Lakini hata hivo hafanyii ushabiki madhehebu ya imamu wake. Anafuata yale ambayo dalili zake ni zenye nguvu ijapokuwa ni kutoka kwa imamu mwingine. Kwa sababu ni mwenye kutaka haki. Ni kama mfano wa Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah, Ibn-ul-Qayyim na wengineo katika wahakiki. Hawafanyi ushabiki. Wanatendea kazi yale yaliyosimama juu ya dalili. Lakini hawatoki nje ya madhehebu manne ambayo ndio madhehebu ya maimamu ambayo wamesoma, wakayajua, kuyahariri na wakayarithi waislamu kizazi kwa kizazi. Kwa hiyo hadai Ijtihaad isiyofungamanishwa. Kwa msemo mwingine ni kwamba hadai kuwa yuko katika safu za wale maimamu wanne; kama Abu Haniyfah, Maalik, ash-Shaafi´iy, Ahmad na al-Awzaa´iy. Lakini wanamsemea uongo. Maneno yake:

“… kwamba mimi nimetoka nje ya Taqliyd.”

Ni kule kukubali maoni ya mwanachuoni bila ya kutambua dalili yake. Taqliyd imegawanyika mafungu mawili:

La kwanza: Kufuata kipofu ambapo mtu akafanyia ushabiki maoni ya mwanachuoni fulani ijapokuwa ni yenye kwenda kinyume na dalili. Shaykh Muhammad na wengineo hawanfanyi hivo.

La pili: Kufuata kwa haki. Ni kama mfano wa kuchukua maoni ya mwanachuoni pale yanapoafikiana na dalili. Huku ni kufuata kwa haki. Huku ni kuwafuata watu wa haki. Kunaitwa pia Taqliyd au kufuata. Maana yake ni moja. Yuusuf (´alayhis-Salaam) alisema:

وَاتَّبَعْتُ مِلَّةَ آبَائِي إِبْرَاهِيمَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ

“Nimefuata mila ya baba zangu; Ibraahiym na Ishaaq na Ya’quub.”[1]

Huku ni kufuata kwa haki.

وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ

“Na wale waliotangulia wa mwanzo miongoni mwa Muhaajiruun na Answaar na wale waliowafuata kwa wema… ”[2]

Huku wanaita ni kufuata. Yule aliye juu ya haki basi sisi tunamfuata.

[1] 12:38

[2] 09:100

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-il-Imaam Mujaddid Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab, uk. 146
  • Imechapishwa: 07/06/2021