106. Khawaarij na Mu´tazilah kuhusu mtenda dhambi kubwa

Kuna mapote mawili yameenda kinyume na hili:

1 – Khawaarij. Wamesema kuwa mtenda dhambi kubwa ni kafiri na atadumishwa Motoni milele.

2 – Mu´tazilah. Wamesema kuwa mtenda dhambi kubwa anatoka nje ya imani. Kwa msemo mwingine sio muumini wala kafiri. Yuko katika daraja kati ya daraja mbili. Aidha atadumishwa Motoni milele.

Tunayaraddi makundi hayo mawili kwa yafuatayo:

1 – Wanaenda kinyume na maandiko ya Qur-aan na Sunnah.

2 – Wanaenda kinyume na maafikiano ya Salaf.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 149
  • Imechapishwa: 15/12/2022