9- Alimsikia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mtu mwingine akisema katika Tashahhud:
اللهم!إني أسألك بأنَّ لك الحمد، لا اله الا أنت، وحدك لا شَريكَ لَكَ ، المنّان، يا بَديعَ السماوات و الأرض!يا ذا الجلال و الإكرام!يا حي يا قيوم!إِني أَسْأَلُك الْجَنَّة وَأَعُوذُ بِكَ مِنَ النَّارِ
“Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba kwa sababu himdi zote ni Zako. Hapana mungu wa haki isipokuwa Wewe, hali ya kuwa upekee huna mshirika. Mwingi wa kuneemesha! Ee mwanzilishi wa mbingu na ardhi! Ee Mwenye utukufu na ukarimu! Ee Uliye hai na Mwenye kusimama kwa dhati Yako! Hakika mimi nakuomba Pepo na najilinda Kwako kutokamana na Moto.”
akasema kuwaambia Maswahabah wake:
“Mnajua alichoomba?” Wakasema: “Allaah na Mtume Wake ndio wanajua zaidi.” Akasema: “Ninaapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mikononi Mwake amemuomba Allaah kwa jina Lake tukufu[1]. Akiombwa kwalo, Anaitika, na akiulizwa kwalo, Anatoa.”[2]
[1] Hapa kuna kufanya Tawassul kwa Allaah kupitia majina Yake mazuri mno na sifa Zake kuu, kitu kilichoamrishwa na Allaah (Ta´ala) pale aliposema:
وَلِلَّـهِ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ فَادْعُوهُ بِهَا
“Allaah ana majina mazuri mno, hivyo basi basi muombeni kwayo.” (07:180)
Ama kuhusu kufanya Tawassul kwa kitu kingine kama vile jaha/heshima, haki na cheo, Abu Haniyfah (Rahimahu Allaah) na wenzake wamesema kuwa imechukizwa, kwa msemo mwingine ni haramu. Kwa masikitiko makubwa utawaona watu wengi leo, wakiwemo wanachuoni wengi, wanapuuzia Tawassul hii iliyowekwa katika Shari´ah ambayo kuna maafikiano juu yake. Unakaribia kutompata yeyote anafanya Tawassul kama hii. Kinyume chake wanajihimiza juu ya Tawassul za ki-Bid´ah ambazo angalau kwa uchache kuna tofauti juu yake. Wameshikamana na hilo kama kwamba hakuna njia nyingine inayofaa. Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) ana kijitabu kizuri juu ya maudhui haya kwa jina ”at-Tawassul wal-Wasiylah”. Kisome! Kina manufaa makubwa na hakina mfano wake katika maudhui haya.
Pia mimi nina kijitabu kinachoitwa ”at-Tawassul, Anwaa´uh wa Ahkaamuh”. Kimeshachapishwa mara mbili. Vilevile ni kitabu chenye manufaa kutokana na maudhui haya na usulubu wake. Ndani yake kunaraddiwa shubuha mpya zinazotoka kwa baadhi ya madakari. Allaah atuongoze sisi na wao.
[2] Abu Daawuud, an-Nasaa’iy, Ahmad, al-Bukhaariy katika ”al-Adab al-Mufrad”, at-Twabaraaniy na Ibn Mandah katika ”at-Tawhiyd” (1-2/70, 1/67 na 2/44) kwa cheni mbili za wapokezi zilizo Swahiyh.
- Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 162
- Imechapishwa: 14/01/2019

Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 162
Imechapishwa: 14/01/2019
https://firqatunnajia.com/106-duaa-ya-sita-kabla-ya-tasliym/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)