105. Dhikr wakati wa kurejea kutoka safarini

  Download

“Aseme:

اللّهُ أَكْـبَر، اللّهُ أَكْـبَر، اللّهُ أَكْـبَر

“Allaah ni mkubwa, Allaah ni mkubwa, Allaah ni mkubwa.”

kila sehemu iliyoinuka kisha aseme:

لا إلهَ إلاّ اللّهُ وَحْـدَهُ لا شريكَ لهُ، لهُ الملكُ ولهُ الحَمْد، وهُوَ على كُلّ شَيءٍ قَـدير، آيِبـونَ تائِبـونَ عابِـدونَ لِرَبِّـنا حـامِـدون، صَدَقَ اللهُ وَعْـدَه، وَنَصَـرَ عَبْـدَه، وَهَزَمَ الأَحْـزابَ وَحْـدَه

“Hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kuwa yupekee hana mshirika, ufalme ni Wake, himdi zote njema ni Zake na Yeye juu ya kila jambo ni muweza. Tunarudi hali ya kuwa tunatubia, tunaabudu na tukiwa ni wenye kumsifu Mola wetu. Amesadikisha Allaah ahadi Yake, amemnusuru mja Wake na amevishinda vikosi peke Yake.”[1]

[1] ”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema hivo pindi anaporejea kutoka vitani au hajj.” al-Bukhaariy (07/163) na Muslim (02/980).

  • Mhusika: Shaykh Sa´iyd bin ´Aliy bin Wahf al-Qahtwaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Huswn-ul-Muslim
  • Imechapishwa: 05/05/2020