Miongoni mwa watu waliolengwa na Qur-aan kwa dhati zao ni Abu Lahab; ´Abdul-´Uzza bin ´Abdil-Muttwalib ami yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na mke wake ambaye ni Umm Jamiyl ´Arwa bint Harb bin Umayyah ambaye ni dada yake Abu Sufyaan. Amesema (Ta´ala):

تَبَّتْ يَدَا أَبِي لَهَبٍ وَتَبَّ مَا أَغْنَىٰ عَنْهُ مَالُهُ وَمَا كَسَبَ  سَيَصْلَىٰ نَارًا ذَاتَ لَهَبٍ وَامْرَأَتُهُ حَمَّالَةَ الْحَطَبِ فِي جِيدِهَا حَبْلٌ مِّن مَّسَدٍ

“Imeteketea mikono miwili ya Abu Lahab na ameteketea. Haikumfaa kitu mali yake na wala yale aliyoyachuma. Ataingia na kuungua moto wenye mwako na mke wake mbebaji kuni za moto. Shingoni mwake kamba ya mtende iliyosokotwa madhubuti.”[1]

Miongoni mwa watu waliolengwa na Sunnah kwa dhati zao ni Abu Twaalib; ´Abd Manaaf bin ´Abdil-Muttwalib. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Watu wa Motoni wenye adhabu ndogo kabisa ni Abu Twaalib. Amevaa viatu viwili ambavyo vinachemsha ubongo wake.”[2]

Ameipokea al-Bukhaariy.

Miongoni mwao vilevile ni ´Amr bin ´Aamir bin al-Lu´ayy al-Khuza´iy. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Nimemuona akiburuza matumbo yake Motoni.”[3]

Ameipokea al-Bukhaariy na wengineo.

[1] 111:01-05

[2] Muslim ndiye amepokea kwa muundo huo (212, 362) na al-Bukhaariy (6561).

[3] al-Bukhaariy (4624) na Muslim (904, 09).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 147-148
  • Imechapishwa: 15/12/2022