Miongoni mwa ambao Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewashuhudilia Pepo ni al-Hasan na al-Husayn na Thaabit bin Qays. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“al-Hasan na al-Husayn ni viongozi wa vijana wa Peponi.”[1]

Ameipokea at-Tirmidhiy ambaye amesema:

“Ni nzuri na Swahiyh.”

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu Thaabit bin Qays:

“Hakika wewe sio katika watu wa Motoni, lakini ni katika watu wa Peponi.”[2]

Ameipokea al-Bukhaariy.

[1] at-Tirmidhiy (3768) na Ahmad (3/166/167). Imaam at-Tirmidhiy (Rahimahu Allaah) amesema ”Hadiyth Hasan na Swahiyh.”

[2] al-Bukhaariy (3613) na Muslim (119, 187).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 146-147
  • Imechapishwa: 15/12/2022