103. Wanaume kujipamba na kuvaa mavazi mazuri kabisa siku ya ´iyd

Anatakiwa kutoka hali ya kutembea na si kupanda kipando. Isipokuwa kama ana udhuru wa kushindwa au umbali. ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia:

“Miongoni mwa Sunnah ni kutoka kwenda katika ´iyd hali ya kutembea.”

Ameipokea at-Tirmidhiy ambaye amesema:

“Hadiyth ni nzuri[1].”

[1] Ndani yake yumo al-Haarith al-A´war na wanazuoni wengi wamemdhoofisha ingawa wengine wameonelea kuwa ni mwenye kuaminika.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majaalis Shahr Ramadhwaan, uk. 225
  • Imechapishwa: 29/03/2024