102. Kula tende witiri kabla ya kwenda kuswali ´Iyd-ul-Fitwr

Miongoni mwa Sunnah ni watu kabla ya kutoka katika ´Iyd-ul-Fitwr wale tende kwa njia ya witiri; tatu, tano au zaidi ya hivo. Ale kwa njia ya witiri. Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa harauki siku ya [´Iyd] al-Fitwr mpaka ale tende na anazila kwa witiri.”

Ameipokea Ahmad na al-Bukhaariy.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majaalis Shahr Ramadhwaan, uk. 225
  • Imechapishwa: 29/03/2024